Psalms 11:4-7


4 a Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu;
Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.
Huwaangalia wana wa watu,
macho yake yanawajaribu.
5 b Bwana huwajaribu wenye haki,
lakini waovu na wanaopenda jeuri,
nafsi yake huwachukia.
6 cAtawanyeshea waovu makaa ya moto mkali
na kiberiti kinachowaka,
upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

7 dKwa kuwa Bwana ni mwenye haki,
yeye hupenda haki.
Wanyofu watauona uso wake.
Copyright information for SwhNEN