Psalms 128

Thawabu Ya Kumtii Bwana

Wimbo wa kwenda juu.

1 aHeri ni wale wote wamchao Bwana,
waendao katika njia zake.
2 bUtakula matunda ya kazi yako;
baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3 cMke wako atakuwa kama mzabibu uzaao
ndani ya nyumba yako;
wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni
kuizunguka meza yako.
4 dHivyo ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye Bwana.

5 e Bwana na akubariki kutoka Sayuni
siku zote za maisha yako,
na uone mafanikio ya Yerusalemu,
6 fnawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako.

Amani iwe juu ya Israeli.
Copyright information for SwhNEN