Psalms 136:10-15


10 aKwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,

Fadhili zake zadumu milele.
11 bNa kuwatoa Israeli katikati yao,

Fadhili zake zadumu milele.
12 cKwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa,

Fadhili zake zadumu milele.

13 dKwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu,

Fadhili zake zadumu milele.
14 eNa kuwapitisha Israeli katikati yake,

Fadhili zake zadumu milele.
15 fLakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu,

Fadhili zake zadumu milele.
Copyright information for SwhNEN