Psalms 22

Kilio Cha Uchungu Na Wimbo Wa Sifa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri.” Zaburi ya Daudi.

1 aMungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa?
Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu?
2 bEe Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu,
hata usiku, sinyamazi.

3 cHata hivyo umesimikwa katika kiti cha enzi kama Uliye Mtakatifu;
wewe ni sifa ya Israeli.
Tafsiri zingine zinasema: uketiye juu ya sifa za Israeli.

4 eKwako wewe baba zetu waliweka tumaini lao,
walikutumaini nawe ukawaokoa.
5 fWalikulilia wewe na ukawaokoa,
walikutegemea wewe nao hawakuaibika.

6 gMimi ni mnyoo wala si mwanadamu,
wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau.
7 hWote wanionao hunidhihaki,
hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao:
8 iHusema, “Anamtegemea Bwana,
basi Bwana na amwokoe.
Amkomboe basi, kwa maana
anapendezwa naye.”

9 jHata hivyo ulinitoa tumboni,
ukanifanya nikutegemee,
hata nilipokuwa ninanyonya
matiti ya mama yangu.
10 kNimekabidhiwa kwako tangu kuzaliwa,
toka tumboni mwa mama yangu
umekuwa Mungu wangu.
11 lUsiwe mbali nami,
kwa maana shida iko karibu
na hakuna wa kunisaidia.

12 mMafahali wengi wamenizunguka,
mafahali wa Bashani wenye nguvu
wamenizingira.
13 nSimba wangurumao wanaorarua mawindo
yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu.
14 oNimemiminwa kama maji,
mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake.
Moyo wangu umegeuka kuwa nta,
umeyeyuka ndani yangu.
15 pNguvu zangu zimekauka kama kigae,
ulimi wangu umegandamana
na kaakaa la kinywa changu,
kwa sababu umenilaza
katika mavumbi ya kifo.
16 qMbwa wamenizunguka,
kundi la watu waovu limenizingira,
wametoboa mikono yangu na miguu yangu.
17 rNaweza kuhesabu mifupa yangu yote,
watu wananikodolea macho na kunisimanga.
18 sWanagawana nguo zangu wao kwa wao,
na vazi langu wanalipigia kura.

19 tLakini wewe, Ee Bwana,
usiwe mbali.
Ee Nguvu yangu,
uje haraka unisaidie.
20 uOkoa maisha yangu na upanga,
uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.
21 vNiokoe kutoka kinywani mwa simba,
niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu.

22 wNitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu,
katika kusanyiko nitakusifu wewe.
23 xNinyi ambao mnamcha Bwana, msifuni!
Ninyi nyote wazao wote wa Yakobo, mheshimuni yeye!
Mcheni yeye, ninyi wazao wote wa Israeli!
24 yKwa maana hakupuuza wala kudharau
mateso ya aliyeonewa;
hakumficha uso wake
bali alisikiliza kilio chake ili amsaidie.

25 zKwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa,
nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe.
26 aaMaskini watakula na kushiba,
wale wamtafutao Bwana watamsifu:
mioyo yenu na iishi milele!
27 abMiisho yote ya dunia itakumbuka
na kumgeukia Bwana,
nazo jamaa zote za mataifa
watasujudu mbele zake,
28 ackwa maana ufalme ni wa Bwana
naye hutawala juu ya mataifa.

29 adMatajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu.
Wote waendao mavumbini
watapiga magoti mbele yake,
wote ambao hawawezi
kudumisha uhai wao.
30 aeWazao wa baadaye watamtumikia yeye;
vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana.
31 afWatatangaza haki yake kwa watu
ambao hawajazaliwa bado,
kwa maana yeye ametenda hili.
Copyright information for SwhNEN