Psalms 37:21-26


21 aWaovu hukopa na hawalipi,
bali wenye haki hutoa kwa ukarimu.
22 bWale wanaobarikiwa na Bwana watairithi nchi,
bali wale anaowalaani watakatiliwa mbali.

23 cKama Bwana akipendezwa na njia ya mtu,
yeye huimarisha hatua zake,
24 dajapojikwaa, hataanguka,
kwa maana Bwana
humtegemeza kwa mkono wake.

25 eNilikuwa kijana na sasa ni mzee,
lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa
au watoto wao wakiombaomba chakula.
26 fWakati wote ni wakarimu na hukopesha bila masharti.
Watoto wao watabarikiwa.
Copyright information for SwhNEN