Psalms 37:3-9


3 aMtumaini Bwana na utende yaliyo mema;
Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.
4 bJifurahishe katika Bwana
naye atakupa haja za moyo wako.

5 cMkabidhi Bwana njia yako,
mtumaini yeye, naye atatenda hili:
6 dYeye atafanya haki yako ingʼae kama mapambazuko,
na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.

7 eTulia mbele za Bwana
na umngojee kwa uvumilivu;
usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,
wanapotekeleza mipango yao miovu.

8 fEpuka hasira na uache ghadhabu,
usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.
9 gKwa maana waovu watakatiliwa mbali,
bali wale wanaomtumaini Bwana watairithi nchi.
Copyright information for SwhNEN