Psalms 40:13-17


13 aEe Bwana, uwe radhi kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
14 bWote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
15 cWale waniambiao, “Aha! Aha!”
wafadhaishwe na iwe aibu yao.
16 dLakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
“Bwana atukuzwe!”

17 eLakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Bwana na anifikirie.
Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu;
Ee Mungu wangu, usikawie.
Copyright information for SwhNEN