Psalms 53:1-3
Uovu Wa Wanadamu
(Zaburi 14)
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi. Utenzi wa Daudi.
1 aMpumbavu anasema moyoni mwake,“Hakuna Mungu.”
Wameharibika, na njia zao ni za uovu kabisa,
hakuna hata mmoja atendaye mema.
2 bMungu anawachungulia wanadamu chini
kutoka mbinguni
aone kama wako wenye akili,
wowote wanaomtafuta Mungu.
3 cKila mmoja amegeukia mbali,
wameharibika wote pamoja,
hakuna atendaye mema.
Naam, hakuna hata mmoja!
Copyright information for
SwhNEN