Psalms 63:3-8
3 aKwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,midomo yangu itakuadhimisha.
4 bNitakusifu siku zote za maisha yangu,
na kwa jina lako nitainua mikono yangu.
5 cNafsi yangu itatoshelezwa
kama kwa wingi wa vyakula;
kwa midomo iimbayo
kinywa changu kitakusifu wewe.
6 dKitandani mwangu ninakukumbuka wewe,
ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.
7 eKwa sababu wewe ndiwe msaada wangu,
chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.
8 fNafsi yangu inaambatana nawe,
mkono wako wa kuume hunishika.
Copyright information for
SwhNEN