Psalms 64:2-8
2 aUnifiche kutokana na shauri la siri la waovu,kutokana na zile kelele za kundi la watenda mabaya.
3 bWananoa ndimi zao kama panga
na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha.
4 cHurusha mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia,
humrushia ghafula bila woga.
5 dKila mmoja humtia moyo mwenzake
katika mipango mibaya;
huzungumza juu ya kuficha mitego yao,
nao husema, “Ni nani ataiona?”
6Hufanya shauri baya la dhuluma na kusema,
“Tumebuni mpango mkamilifu!”
Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila.
7Bali Mungu atawapiga kwa mishale,
nao ghafula wataangushwa.
8 eAtageuza ndimi zao wenyewe dhidi yao
na kuwaleta kwenye maangamizi;
wote wawaonao watatikisa vichwa vyao
kwa dharau.
Copyright information for
SwhNEN