Psalms 80:8-16


8 aUlileta mzabibu kutoka Misri,
ukawafukuza mataifa, ukaupanda.
9Uliandaa shamba kwa ajili yake,
mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.
10Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,
matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.
11 bMatawi yake yalienea mpaka Baharini,
Huenda inamaanisha Bahari ya Mediterania.

machipukizi yake mpaka kwenye Mto.
Yaani Mto Frati.


12 eMbona umebomoa kuta zake
ili wote wapitao karibu
wazichume zabibu zake?
13 fNguruwe mwitu wanauharibu
na wanyama wa kondeni hujilisha humo.
14 gTurudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote!
Tazama chini kutoka mbinguni na uone!
Linda mzabibu huu,
15 hmche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume,
mwana uliyemlea
kwa ajili yako mwenyewe.

16 iMzabibu wako umekatwa, umechomwa moto,
unapowakemea, watu wako huangamia.
Copyright information for SwhNEN