Psalms 89:29-37
29 aNitaudumisha uzao wake milele,kiti chake cha enzi kama mbingu zinavyodumu.
30 b“Kama wanae wataacha amri yangu
na wasifuate sheria zangu,
31kama wakihalifu maagizo yangu
na kutoshika amri zangu,
32 cnitaadhibu dhambi yao kwa fimbo,
uovu wao kwa kuwapiga,
33 dlakini sitauondoa upendo wangu kwake,
wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe.
34 eMimi sitavunja agano langu
wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka.
35 fMara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu,
nami sitamdanganya Daudi:
36 gkwamba uzao wake utaendelea milele,
na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;
37 hkitaimarishwa milele kama mwezi,
shahidi mwaminifu angani.”
Copyright information for
SwhNEN