Psalms 90:3-8


3 aHuwarudisha watu mavumbini,
ukisema, “Rudini mavumbini, enyi wanadamu.”
4 bKwa maana kwako miaka elfu
ni kama siku moja iliyokwisha pita,
au kama kesha la usiku.
5 cUnawatowesha wanadamu katika usingizi wa kifo,
nao ni kama majani machanga ya asubuhi:
6 dingawa asubuhi yanachipua,
ifikapo jioni huwa yamenyauka na kukauka.

7Tumeangamizwa kwa hasira yako
na tumetishwa kwa ghadhabu yako.
8 eUmeyaweka maovu yetu mbele yako,
dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako.
Copyright information for SwhNEN