Psalms 91:3-11


3 aHakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,
na maradhi ya kuambukiza ya kuua.
4 bAtakufunika kwa manyoya yake,
chini ya mbawa zake utapata kimbilio,
uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.
5 cHutaogopa vitisho vya usiku,
wala mshale urukao mchana,
6wala maradhi ya kuambukiza
yanayonyemelea gizani,
wala tauni iharibuyo adhuhuri.
7Ijapo watu elfu wataangukia kando yako,
kumi elfu mkono wako wa kuume,
lakini haitakukaribia wewe.
8 dUtatazama tu kwa macho yako
na kuona adhabu ya waovu.

9Kama ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako:
naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu,
10 ebasi hakuna madhara yatakayokupata wewe,
hakuna maafa yataikaribia hema yako.
11 fKwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako,
wakulinde katika njia zako zote.
Copyright information for SwhNEN