Revelation of John 12:9-10

9 aLile joka kuu likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au Shetani, aupotoshaye ulimwengu wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake.

Ushindi Mbinguni Watangazwa

10 bKisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema:

“Sasa wokovu na uweza na Ufalme wa Mungu wetu umekuja
na mamlaka ya Kristo wake.
Kwa kuwa ametupwa chini
mshtaki wa ndugu zetu,
anayewashtaki mbele za Mungu
usiku na mchana.
Copyright information for SwhNEN