Zechariah 9:1-4
Hukumu Juu Ya Adui Za Israeli
1Neno:aNeno la Bwana liko kinyume na nchi ya Hadraki
na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika,
kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote
za Israeli yako kwa Bwana,
2 bpia juu ya Hamathi inayopakana nayo,
juu ya Tiro na Sidoni,
ingawa wana ujuzi mwingi sana.
3 cTiro amejijengea ngome imara,
amelundika fedha kama mavumbi
na dhahabu kama taka za mitaani.
4 dLakini Bwana atamwondolea mali zake
na kuuangamiza uwezo wake wa baharini,
naye atateketezwa kwa moto.
Copyright information for
SwhNEN