1 Chronicles 1:43-54
Watawala Wa Edomu
(Mwanzo 36:31-43)
43 aHawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.
44Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
45 bYobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
46 cHushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
47Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
48 dSamla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.
49Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
50 eBaal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. 51 fNaye Hadadi pia akafa.
Wakuu wa Edomu walikuwa:
Timna, Alva, Yethethi, 52Oholibama, Ela, Pinoni, 53Kenazi, Temani, Mibsari, 54Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.
Copyright information for
SwhNEN