1 Chronicles 14:11-16
11 aHivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu, ▼▼Maana yake ni Bwana Afurikae.
akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu. 12 cWafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto. 13 dKwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde; 14 ehivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi. 15Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.” 16 fKwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri.
Copyright information for
SwhNEN