1 Kings 10:26-29

26 aSolomoni akakusanya magari ya vita na farasi. Alikuwa na magari 1,400 na farasi 12,000, ambayo aliyaweka katika miji ya magari na mengine akawa nayo huko Yerusalemu. 27 bMfalme akafanya fedha kuwa kitu cha kawaida kama mawe huko Yerusalemu, mierezi akaifanya kuwa mingi kama mikuyu vilimani. 28Farasi wa Solomoni waliletwa kutoka Misri na kutoka Kue.
Yaani Kilikia ilioko Syria.
Wafanyabiashara wa mfalme waliwanunua kutoka Kue.
29 dWaliagiza magari kutoka Misri kwa bei ya shekeli 600 za fedha
Shekeli 600 za fedha ni sawa na kilo 7.
na farasi kwa shekeli 150.
Shekeli 150 za fedha ni sawa na kilo 1.7.
Pia waliwauza nje kwa wafalme wote wa Wahiti na wa Waaramu.
Waaramu hapa ina maana ya Washamu.


Copyright information for SwhNEN