1 Samuel 31:11-13
11 aWatu wa Yabeshi-Gileadi waliposikia yale Wafilisti walichomfanyia Sauli, 12 bmashujaa wao wote wakaenda usiku hadi Beth-Shani. Wakauchukua mwili wa Sauli na miili ya wanawe kutoka kwenye ukuta wa Beth-Shani na kurudi hadi Yabeshi, mahali ambapo waliiteketeza kwa moto. 13 cKisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba.
Copyright information for
SwhNEN