‏ 2 Kings 21:19-26

Amoni Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 33:21-25)

19Amoni alikuwa na miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. Mamaye aliitwa Meshulemethi binti Haruzi, kutoka Yotba. 20 aAkatenda maovu machoni mwa Bwana, kama baba yake Manase alivyofanya. 21Akaenenda katika njia zote za baba yake, akaabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu na kuzisujudia. 22 bAkamwacha Bwana, Mungu wa baba zake, wala hakuenenda katika njia za Bwana.

23Watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, nao wakamuulia kwake nyumbani. 24Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamefanya hila dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.

25Matukio mengine ya utawala wa Amoni na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 26Akazikwa kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza. Naye Yosia mwanawe akawa mfalme baada yake.

Copyright information for SwhNEN