b2Sam 12:1; 1Fal 1:8, 22; 1Nya 29:29; 2Nya 9:29; 2Sam 5:11; 1Fal 3:1; 7:1-7; 9:1; 2Nya 8:1; Yer 22:14; Hag 1:4; Kut 26:1; Za 132:3; Mdo 7:45-46; Kut 40:21
fKum 23:14; 2Sam 5:2; 1Fal 8:27; Isa 66:1; Law 26:11; Za 78:72; Eze 34:2, 15, 23; Mt 2:6; Mdo 20:28; 1Pet 5:2
iKut 15:17; Isa 5:1-7; 2Fal 21:8; 2Nya 33:8; Za 89:22-23; 147:14; Isa 54:14; 60:18; Za 44:2; 80:8; Yer 24:6; Amo 9:15
jAmu 2:16; 1Sam 12:9-11; 1Fal 2:24; 1Sam 25:28; Za 89:35-37; Lk 1:32-33; Mdo 13:22-23; 2Tim 2:8; Kut 1:21; Isa 7:2
lKum 12:5; 1Fal 5:5; 6:12; 8:19, 29; Kum 16:11; 2Fal 21:4, 7; Mit 25:5; Dan 7:27; Mwa 9; 16; 2Sam 22:51; 1Fal 2:4, 45; 1Nya 22; 10; 28:6; 2Nya 6:16; 7:18; 13:5; 21:7; Za 89:3-4; Isa 9:7; 16:5; Yer 17:25; 33:17-21
mZa 2:7; 89:26; Yer 3:19; Mt 3:17; Yn 1:49; 2Kor 6:18; Ebr 1:5; Ufu 21:7; Kum 8:5; 1Fal 11:34; 1Nya 22:10; Ebr 12:7; Za 89:30-33; Mit 13:24
n1Fal 2:4; 6:12; 8:25; 9:5; 11:13; 2Fal 19:34; 2Nya 6:16; 7:18; 21:7; Za 89:34; Yer 33; 17; 1Sam 13:13; 15:28; 16:14; 7:16; Za 89:36-37; Lk 1:33; Za 9:7; 93:2; 103:19
2 Samuel 7
Ahadi Ya Mungu Kwa Daudi
(1 Nyakati 17:1-15)
1 aBaada ya mfalme kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, naye Bwana akiwa amemstarehesha pande zote mbali na adui zake, 2 bakamwambia nabii Nathani, “Mimi hapa, ninaishi katika jumba la kifalme la mierezi, wakati Sanduku la Mungu limebaki katika hema.”3 cNathani akamjibu mfalme, “Lolote ulilo nalo moyoni, endelea ukalifanye, kwa maana Bwana yu pamoja nawe.”
4Usiku ule neno la Bwana likamjia Nathani, kusema:
5 d“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Je, ewe ndiwe wa kunijengea mimi nyumba ili nikae ndani yake? 6 eSijakaa ndani ya nyumba tangu siku niliyowaleta Waisraeli kutoka Misri hadi leo. Nimekuwa nikitembea kutoka mahali pamoja hadi mahali pengine ndani ya hema kama makao yangu. 7 fPopote nilipotembea pamoja na Waisraeli wote, je, nimewahi kumwambia kiongozi wao yeyote niliyemwamuru kuwachunga watu wangu Israeli, “Kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?” ’
8 g“Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: Nilikutoa wewe kutoka machungani na kutoka kuandama kundi la kondoo na mbuzi ili kuwaongoza watu wangu Israeli. 9 hNimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani. 10 iNami nitawapatia watu wangu Israeli mahali niwapande humo ili kwamba wawe na nyumbani kwao wenyewe wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni, 11 jna kama walivyofanya tangu mwanzo wakati nilipowaweka viongozi juu ya watu wangu Israeli. Pia nitawapa raha mbele ya adui zenu wote.
“ ‘Bwana akuambia kwamba Bwana mwenyewe atakujengea nyumba. 12 kSiku zako zitakapokwisha nawe ulale pamoja na baba zako, nitainua mzao wako aingie mahali pako, ambaye atatoka viunoni mwako, nami nitauimarisha ufalme wake. 13 lYeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, nami nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele. 14 mNitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Atakapokosea nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu, kwa adhabu ya kupigwa na wanadamu. 15 nLakini upendo wangu kamwe hautaondolewa kwake, kama nilivyouondoa kwa Sauli, niliyemwondoa atoke mbele yako. 16Nyumba yako na ufalme wako utadumu milele mbele zangu, kiti chako cha enzi kitafanywa imara milele.’ ”
17Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.
Maombi Ya Daudi
(1 Nyakati 17:16-27)
18 oNdipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema:“Ee Bwana Mwenyezi, mimi ni nani, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo? 19 pNaam, kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Bwana Mwenyezi, wewe umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Je, hii ndiyo njia yako ya kawaida ya kushughulika na mwanadamu, Ee Bwana Mwenyezi?
20 q“Je, Daudi aweza kukuambia nini zaidi? Kwa maana unamjua mtumishi wako, Ee Bwana Mwenyezi. 21 rKwa ajili ya neno lako na kwa mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa na kulifanya lijulikane na lifahamike kwa mtumishi wako.
22 s“Tazama jinsi ulivyo mkuu, Ee Bwana Mwenyezi! Hakuna mwingine kama wewe, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe, 23 tNaye ni nani aliye kama watu wako Israeli, taifa pekee duniani ambalo Mungu alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe, na kujifanyia jina mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa na miungu yao mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri? 24 uUmeimarisha watu wako Israeli hasa kama watu wako mwenyewe milele, nawe, Ee Bwana, umekuwa Mungu wao.
25 v“Basi sasa, Bwana, ukaitimize ahadi uliyosema kuhusu mtumishi wako na nyumba yake milele. Fanya kama ulivyoahidi, 26 wili kwamba jina lako litukuke milele. Ndipo watu watasema, ‘Bwana Mwenye Nguvu Zote ni Mungu juu ya Israeli!’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itakuwa imara mbele zako.
27“Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, umelifunua hili kwa mtumishi wako, ukisema, ‘Nitakujengea nyumba.’ Hivyo mtumishi wako amepata ujasiri kukuletea dua hii. 28 xEe Bwana Mwenyezi, wewe ndiwe Mungu! Maneno yako ndiyo kweli, nawe umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri. 29 ySasa naomba uwe radhi kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu mbele zako milele, kwa maana wewe, Ee Bwana Mwenyezi, umesema, na kwa baraka zako nyumba ya mtumishi wako itaendelea kubarikiwa milele.”
Copyright information for
SwhNEN