Amos 3
Mashahidi Waitwa Dhidi Ya Israeli
1 aSikilizeni neno hili alilosema Bwana dhidi yenu, enyi watu wa Israeli, dhidi ya jamaa nzima niliowapandisha toka Misri:2 b“Ni ninyi tu niliowachagua
kati ya jamaa zote za dunia;
kwa hiyo nitawaadhibu
kwa ajili ya dhambi zenu zote.”
3Je, watu wawili hutembea pamoja
wasipokubaliana kufanya hivyo?
4 cJe, simba hunguruma katika kichaka
wakati hana mawindo?
Aweza kuvuma katika pango
wakati ambao hajakamata chochote?
5Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhini
ambapo hajategewa chambo?
Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhini
wakati ambapo hakuna chochote cha kunasa?
6 dJe, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari,
watu hawatetemeki?
Mji upatwapo na maafa,
je, si Bwana amesababisha?
7 eHakika Bwana Mwenyezi hatafanya neno lolote
bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.
8 fSimba amenguruma:
je, ni nani ambaye hataogopa?
Bwana Mwenyezi ametamka:
je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii?
9 gTangazeni katika ngome za Ashdodi
na katika ngome za Misri:
“Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria;
angalieni wingi wa wasiwasi ulio ndani yake,
na uonevu ulio miongoni mwa watu wake.”
10 h Bwana asema: “Hawajui kutenda lililo jema,
wale ambao hujilundikia nyara
na vitu vilivyotekwa katika ngome zao.”
11 iKwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:
“Adui ataizingira nchi;
ataangusha chini ngome zenu
na kuteka nyara maboma yenu.”
12 jHili ndilo asemalo Bwana:
“Kama vile mchungaji aokoavyo kinywani mwa simba
vipande viwili tu vya mfupa wa mguu
au kipande cha sikio,
hivyo ndivyo Waisraeli watakavyookolewa,
wale wakaao Samaria
kwenye kingo za vitanda vyao,
na katika Dameski
kwenye viti vyao vya fahari.”
13“Sikia hili na ushuhudie dhidi ya nyumba ya Yakobo,” asema Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.
14 k“Siku nitakapomwadhibu Israeli kwa sababu ya dhambi zake,
nitaharibu madhabahu za Betheli;
pembe za madhabahu zitakatiliwa mbali
na kuanguka chini.
15 lNitabomoa nyumba ya wakati wa masika,
pamoja na nyumba ya wakati wa kiangazi;
nyumba zilizonakshiwa kwa pembe za ndovu
na majumba makubwa ya fahari yatabomolewa,”
asema Bwana.
Copyright information for
SwhNEN