a Ay 5:14; Mk 15:33; Eze 32:7; Amo 4:13; 5:8; Isa 13:10; 59:9-10; Yer 15:9; Mik 3:6; 1The 5:2, 3; Mt 27:45
Amos 8:9-11
9 a“Katika siku ile,” asema Bwana Mwenyezi,“Nitalifanya jua litue alasiri na kuifanya dunia
iwe giza wakati wa mchana mwangavu.
10 bNitageuza sikukuu zenu za kidini kuwa maombolezo,
na kuimba kwenu kote kuwe kilio.
Nitawafanya ninyi nyote mvae nguo ya gunia
na kunyoa nywele zenu.
Nitaufanya wakati ule uwe kama wa kuombolezea mwana wa pekee,
na mwisho wake kama siku ya uchungu.
11 c“Siku zinakuja,” asema Bwana Mwenyezi,
“wakati nitakapotuma njaa katika nchi yote:
si njaa ya chakula wala kiu ya maji,
lakini njaa ya kusikia maneno ya Bwana.
Copyright information for
SwhNEN