‏ Daniel 4:34-35

34 aMwisho wa huo wakati, mimi Nebukadneza, niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, nazo fahamu zangu zikanirudia. Ndipo nikamsifu Yeye Aliye Juu Sana, nikamheshimu na kumhimidi yeye aishiye milele.

Utawala wake ni utawala wa milele;
ufalme wake hudumu kutoka kizazi na kizazi.
35 bMataifa yote ya dunia
yanahesabiwa kuwa si kitu.
Hufanya kama atakavyo
kwa majeshi ya mbinguni,
na kwa mataifa ya dunia.
Hakuna anayeweza kuuzuia mkono wake
au kumwambia, “Umefanya nini wewe?”
Copyright information for SwhNEN