‏ Ecclesiastes 4:4-6

4Tena nikaona kuwa kazi zote na mafanikio yote huchipuka kutokana na wivu wa mtu kwa jirani yake. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo.

5 aMpumbavu hukunja mikono yake
na kujiangamiza mwenyewe.
6 bAfadhali konzi moja pamoja
na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu
na kukimbiza upepo.
Copyright information for SwhNEN