Exodus 30:23-30
23 a“Chukua vikolezi bora vifuatavyo: shekeli 500 ▼▼Shekeli 500 ni sawa na kilo 6.
za manemane ya maji, shekeli 250 ▼▼Shekeli 250 ni sawa na kilo 3.
za mdalasini wenye harufu nzuri, shekeli 250 za miwa yenye harufu nzuri, 24 dshekeli 500 za aina nyingine ya mdalasini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, pia hini ▼▼Hini moja ni sawa na lita 4.
ya mafuta ya zeituni. 25 fVitengeneze vikolezi hivi kuwa mafuta matakatifu ya upako yenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Yatakuwa mafuta matakatifu ya upako. 26 gKisha yatumie kupaka hilo Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda, 27meza na vifaa vyake vyote, kinara cha taa na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba, 28madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote na sinia pamoja na kitako chake. 29 hUtaviweka wakfu ili viwe vitakatifu sana na kila kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu. 30 i“Mtie Aroni na wanawe mafuta na uwaweke wakfu ili waweze kunitumikia katika kazi ya ukuhani.
Copyright information for
SwhNEN