Ezra 10

Toba Ya Watu

1 aWakati Ezra alipokuwa anaomba na kuungama, huku akilia na kujitupa chini mbele ya nyumba ya Mungu, umati mkubwa wa Waisraeli, wanaume, wanawake na watoto walikusanyika kumzunguka. Nao pia wakalia sana. 2 bKisha Shekania mwana wa Yehieli, mmoja wa wazao wa Elamu, akamwambia Ezra, “Tumekosa uaminifu kwa Mungu wetu kwa kuoa wanawake wa kigeni kutoka mataifa yanayotuzunguka. Lakini pamoja na hili, bado liko tumaini kwa ajili ya Israeli. 3 cSasa na tufanye agano mbele za Mungu wetu kuwafukuza hawa wanawake wote pamoja na watoto wao, kulingana na maonyo ya bwana wangu pamoja na wale ambao wanaogopa amri za Mungu wetu. Hili na lifanyike sawasawa na hii Sheria. 4 dInuka, suala hili lipo mikononi mwako. Sisi tutaungana nawe, uwe na ujasiri ukatende hili.”

5 eBasi Ezra akainuka na kuwaapisha makuhani viongozi, Walawi na Israeli yote kufanya lile lililokuwa limependekezwa. Nao wakaapa. 6 fNdipo Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu akaenda kwenye chumba cha Yehohanani mwana wa Eliashibu. Wakati alipokuwa hapo, hakula chakula wala hakunywa maji, kwa sababu aliendelea kuomboleza kuhusu kukosa uaminifu kwa watu wa uhamishoni.

7Ndipo lilipotolewa tangazo Yuda yote na Yerusalemu kwa watu wote waliokuwa uhamishoni kukusanyika Yerusalemu. 8 gYeyote ambaye hangejitokeza kwa muda wa siku tatu angepoteza mali yake yote, kulingana na uamuzi wa maafisa na wazee, naye mtu huyo angefukuzwa kutoka kusanyiko la watu waliokuwa uhamishoni.

9 hKatika muda wa siku tatu, watu wote wa Yuda na Benyamini wakawa wamekusanyika huko Yerusalemu. Kwenye siku ya ishirini ya mwezi wa tisa, watu wote walikuwa wameketi ndani ya uwanja mbele ya nyumba ya Mungu, wakiwa na majonzi mno kwa tukio hilo na kwa sababu ya mvua kubwa. 10Ndipo Kuhani Ezra aliposimama akawaambia, “Mmekosa uaminifu, mmeoa wanawake wa kigeni, mkaongezea hatia ya Israeli. 11 iSasa tubuni kwa Bwana, Mungu wa baba zenu mkafanye mapenzi yake. Jitengeni na mataifa wanaowazunguka na wake zenu wa kigeni.”

12 jKusanyiko lote likajibu kwa sauti kubwa: “Uko sawa kabisa! Ni lazima tufanye kama unavyosema. 13Lakini hapa pana watu wengi na ni wakati wa mvua, hivyo hatuwezi kusimama nje. Hata hivyo, shauri hili haliwezi kumalizika kwa siku moja au mbili, kwa sababu tumefanya dhambi kubwa katika jambo hili. 14 kMaafisa wetu na wafanye kwa niaba ya kusanyiko lote. Kisha kila mmoja katika miji yetu ambaye ameoa mwanamke wa kigeni aje kwa wakati uliopangwa, akiwa pamoja na wazee na waamuzi wa kila mji, hadi hasira kali ya Mungu wetu katika shauri hili itakapoondolewa kwetu.” 15 lYonathani mwana wa Asaheli na Yazeya mwana wa Tikwa peke yao, wakiungwa mkono na Meshulamu na Shabethai Mlawi, ndio waliopinga jambo hili.

16Basi watu wa uhamishoni wakafanya kama ilivyokuwa imependekezwa. Kuhani Ezra akachagua wanaume waliokuwa viongozi wa jamaa, mmoja kutoka kila mgawanyo wa jamaa, nao wote wakachaguliwa kwa majina. Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kumi waliketi kuchunguza mashauri hayo. 17Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wakawa wamemaliza kushughulikia wanaume wote waliokuwa wameoa wanawake wa kigeni.

Wenye Hatia Ya Kuoa Wake Wa Kigeni

18 mMiongoni mwa wazao wa makuhani, wafuatao walikuwa wameoa wanawake wa kigeni:

Kutoka wazao wa Yeshua mwana wa Yosadaki na ndugu zake: Maaseya, Eliezeri, Yaribu na Gedalia.
19 n(Wote walitoa nadhiri kwa kuandika kwa mikono yao kuwafukuza wake zao, kwa hatia yao, kila mmoja akatoa kondoo dume kutoka kundini mwake kama sadaka ya hatia.)
20 oKutoka wazao wa Imeri:
Hanani na Zebadia.
21 pKutoka wazao wa Harimu:
Maaseya, Eliya, Shemaya, Yehieli na Uzia.
22 qKutoka wazao wa Pashuri:
Elioenai, Maaseya, Ishmaeli, Nethaneli, Yozabadi na Elasa.

23 rMiongoni mwa Walawi:
Yozabadi, Shimei, Kelaya (ndiye Kelita), Pethahia, Yuda na Eliezeri.
24 sKutoka waimbaji:
Eliashibu.
Kutoka mabawabu:
Shalumu, Telemu na Uri.

25 tMiongoni mwa Waisraeli wengine:

Kutoka wazao wa Paroshi:
Ramia, Izia, Malkiya, Miyamini, Eleazari, Malkiya na Benaya.
26Kutoka wazao wa Elamu:
Matania, Zekaria, Yehieli, Abdi, Yeremothi na Eliya.
27Kutoka wazao wa Zatu:
Elioenai, Eliashibu, Matania, Yeremothi, Zabadi na Aziza.
28Kutoka uzao wa Bebai:
Yehohanani, Hanania, Zabai na Athlai.
29Kutoka wazao wa Bani:
Meshulamu, Maluki, Adaya, Yashubu, Sheali na Yeremothi.
30Kutoka wazao wa Pahath-Moabu:
Adna, Kelali, Benaya, Maaseya, Matania, Bezaleli, Binui na Manase.
31Kutoka wazao wa Harimu:
Eliezeri, Ishiya, Malkiya, Shemaya, Shimeoni,
32Benyamini, Maluki, na Shemaria.
33Kutoka wazao wa Hashumu:
Matenai, Matata, Zabadi, Elifeleti, Yeremai, Manase na Shimei.
34Kutoka wazao wa Bani:
Maadai, Amramu, Ueli,
35Benaya, Bedeya, Keluhi, 36Vania, Meremothi, Eliashibu, 37Matania, Matenai na Yaasu.
38Kutoka wazao wa Binui:
Shimei,
39Shelemia, Nathani, Adaya, 40Maknadebai, Shashai, Sharai, 41Azareli, Shelemia, Shemaria, 42Shalumu, Amaria na Yosefu.
43 uKutoka wazao wa Nebo:
Yeieli, Matithia, Zabadi, Zebina, Yadai, Yoeli na Benaya.

44 vHawa wote walikuwa wameoa wanawake wa kigeni, na baadhi yao walikuwa wamezaa nao watoto.

Copyright information for SwhNEN