Galatians 5
Uhuru Ndani Ya Kristo
1 aKristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa.2 bSikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia chochote. 3 cNamshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote. 4 dNinyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu. 5 eKwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki. 6 fKwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.
7 gMlikuwa mkipiga mbio vizuri. Ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 8 hUshawishi wa namna hiyo haukutokana na yule anayewaita. 9 i“Chachu kidogo huchachua donge zima.” 10 jNina hakika katika Bwana kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani. 11 kLakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini bado ninateswa? Katika hiyo hali basi, kwazo la msalaba limeondolewa. 12 lLaiti hao wanaowavuruga wangejihasi wao wenyewe!
13 mNdugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo. 14 nKwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 15Kama mkiumana na kutafunana, angalieni, msije mkaangamizana.
Maisha Ya Kiroho
16 oKwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 pKwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka. 18 qLakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.19 rBasi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, 20kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 shusuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.
22 tLakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria. 24Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake. 25Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho. 26 uTusijisifu bure, tukichokozana na kuoneana wivu.
Copyright information for
SwhNEN