Isaiah 1:11-16
11 a Bwana anasema, “Wingi wa sadaka zenu,ni kitu gani kwangu?
Ninazo sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi,
za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona.
Sipendezwi na damu za mafahali
wala za wana-kondoo na mbuzi.
12 bMnapokuja kujihudhurisha mbele zangu,
ni nani aliyewataka ninyi mfanye hivyo,
huku kuzikanyaga nyua zangu?
13 cAcheni kuniletea sadaka zisizokuwa na maana!
Uvumba wenu ni chukizo kwangu.
Miandamo ya Mwezi, Sabato na makusanyiko ya ibada:
siwezi kuvumilia makusanyiko yenu maovu.
14 dSikukuu zenu za Miandamo ya Mwezi, na sikukuu zenu zilizoamriwa:
moyo wangu unazichukia.
Zimekuwa mzigo kwangu,
nimechoka kuzivumilia.
15 eMnaponyoosha mikono yenu katika maombi,
nitaficha macho yangu nisiwaone;
hata mkiomba maombi mengi
sitasikiliza.
Mikono yenu imejaa damu;
16 fjiosheni na mkajitakase.
Yaondoeni matendo yenu maovu
mbele zangu!
Acheni kutenda mabaya,
Copyright information for
SwhNEN