Isaiah 30:12-14
12 aKwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:“Kwa sababu mmekataa ujumbe huu,
mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu,
13 bdhambi hii itakuwa kwenu
kama ukuta mrefu,
wenye ufa na wenye kubetuka,
ambao unaanguka ghafula,
mara moja.
14 cUtavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo
ukipasuka pasipo huruma
ambapo katika vipande vyake
hakuna kipande kitakachopatikana
kwa kuukulia makaa kutoka jikoni
au kuchotea maji kisimani.”
Copyright information for
SwhNEN