Isaiah 38:1-8
Kuugua Kwa Mfalme Hezekia
(2 Wafalme 20:1-11; 2 Nyakati 32:24-26)
1 aKatika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”2Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana: 3 b“Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.
4 cNdipo neno la Bwana likamjia Isaya, kusema: 5 d“Nenda ukamwambie Hezekia, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako. Nitakuongezea miaka kumi na mitano katika maisha yako. 6 eNami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mkononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu.
7 f“ ‘Hii ndiyo ishara ya Bwana kwako ya kwamba Bwana atafanya kile alichoahidi: 8 gNitafanya kivuli cha jua kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi kirudi nyuma madaraja kumi.’ ” Hivyo jua likarudi nyuma madaraja kumi ambayo lilikuwa limeshuka.
Copyright information for
SwhNEN