Isaiah 41:22-26
22 a“Leteni sanamu zenu zituambieni nini kitakachotokea.
Tuambieni mambo ya zamani yalikuwa nini,
ili tupate kuyatafakari
na kujua matokeo yake ya mwisho.
Au tutangazieni mambo yatakayokuja,
23 btuambieni ni nini kitakachotokea baadaye,
ili tupate kujua kuwa ninyi ni miungu.
Fanyeni jambo lolote zuri au baya,
ili tupate kutishika na kujazwa na hofu.
24 cLakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa,
na kazi zenu hazifai kitu kabisa;
yeye awachaguaye ni chukizo sana.
25 d“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini,
naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu.
Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope,
kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia.
26 eNi nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua,
au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’?
Hakuna aliyenena hili,
hakuna aliyetangulia kusema hili,
hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu.
Copyright information for
SwhNEN