Isaiah 48:9-11
9 aKwa ajili ya Jina langu mwenyeweninaichelewesha ghadhabu yangu,
kwa ajili ya sifa zangu nimeizuia isikupate,
ili nisije nikakukatilia mbali.
10 bTazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha,
nimekujaribu katika tanuru ya mateso.
11 cKwa ajili yangu mwenyewe,
kwa ajili yangu mwenyewe, nafanya hili.
Jinsi gani niliache Jina langu lichafuliwe?
Sitautoa utukufu wangu kwa mwingine.
Copyright information for
SwhNEN