Isaiah 8

Ashuru, Chombo Cha Bwana

1 a Bwana akaniambia, “Chukua gombo kubwa, uandike juu yake kwa kalamu ya kawaida jina: Maher-Shalal-Hash-Bazi.
Maher-Shalal-Hash-Bazi maana yake ni Haraka kuteka nyara, Upesi kwenye hizo nyara.
2 cNami nitawaita kuhani Uria, na Zekaria mwana wa Yeberekia kama mashahidi wangu waaminifu.”

3 dKisha nikaenda kwa nabii mke, naye akapata mimba, akazaa mwana. Kisha Bwana akaniambia, “Mwite huyo mtoto Maher-Shalal-Hash-Bazi. 4 eKabla mtoto hajaweza kusema ‘Baba yangu’ au ‘Mama yangu,’ utajiri wa Dameski na nyara za Samaria zitachukuliwa na mfalme wa Ashuru.”

5 Bwana akasema nami tena:

6 f“Kwa sababu watu hawa wamekataa maji ya Shilo yatiririkayo taratibu
wakamfurahia Resini na mwana wa Remalia,
7 gkwa hiyo Bwana yu karibu kuleta dhidi yao
mafuriko makubwa ya Mto:
Yaani Frati.

yaani mfalme wa Ashuru na fahari yake yote.
Yatafurika juu ya mifereji yake yote,
yatamwagikia juu ya kingo zake zote,
8 ina kufika hadi Yuda, yakizunguka kwa kasi juu yake,
yakipita katikati na yakifika hadi shingoni.
Mabawa yake yaliyokunjuliwa
yatafunika upana wa nchi yako,
Ee Imanueli!”
Imanueli maana yake Mungu yu pamoja nasi.


9 kInueni kilio cha vita, enyi mataifa,
na mkavunjwevunjwe!
Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali.
Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!
10 lWekeni mikakati yenu, lakini itashindwa;
fanyeni mipango yenu, lakini haitafanikiwa,
kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
Kiebrania ni Imanueli.

Mwogope Mungu

11 n Bwana alisema nami mkono wake wenye nguvu ukiwa juu yangu, akinionya nisifuate njia za taifa hili. Akasema:

12 o“Usiite fitina kila kitu ambacho watu hawa hukiita fitina,
usiogope kile wanachokiogopa,
wala usikihofu.
13 p Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye peke yake
ikupasaye kumheshimu kuwa mtakatifu,
ndiye peke yake utakayemwogopa,
ndiye peke yake utakayemhofu,
14 qnaye atakuwa mahali patakatifu;
lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa
jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa
na mwamba wa kuwaangusha.
Kwa watu wa Yerusalemu,
atakuwa mtego na tanzi.
15 rWengi wao watajikwaa;
wataanguka na kuvunjika,
watategwa na kunaswa.”

16 sFunga ushuhuda na kutia muhuri sheria
miongoni mwa wanafunzi wangu.
17 tNitamngojea Bwana,
ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake.
Nitaliweka tumaini langu kwake.
18 uNiko hapa, pamoja na watoto ambao Bwana amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayeishi juu ya Mlima Sayuni.

19 vWakati watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunongʼona na kunungʼunika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai? 20 wKwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko. 21 xWatazunguka katika nchi yote, wakiwa na dhiki na njaa. Watakapotaabika kwa njaa, watapatwa na hasira kali, nao, wakiwa wanatazama juu, watamlaani mfalme wao na Mungu wao. 22 yKisha wataangalia duniani na kuona tu dhiki na giza, hofu na huzuni tupu, nao watasukumiwa kwenye giza nene kabisa.

Copyright information for SwhNEN