Job 26

Hotuba Ya Tisa Ya Ayubu

Ayubu Anajibu: Utukufu Wa Mungu Hauchunguziki

1Kisha Ayubu akajibu:

2 a“Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!
Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!
3 bNi shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?
Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha!
4 cNi nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?
Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?

5 d“Wafu wako katika maumivu makuu,
wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake.
6 eMauti
Yaani Kuzimu; Kiebrania ni Sheol.
iko wazi mbele za Mungu;
Uharibifu
Kwa Kiebrania ni Abadon.
haukufunikwa.
7 h iHutandaza anga la kaskazini mahali patupu;
naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu.
8 jHuyafungia maji kwenye mawingu yake,
hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
9 kHuufunika uso wa mwezi mpevu,
akitandaza mawingu juu yake.
10 lAmechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji,
ameweka mpaka wa nuru na giza.
11 mNguzo za mbingu nazo zatetemeka,
zinatishika anapozikemea.
12 nKwa nguvu zake aliisukasuka bahari;
kwa hekima yake alimkata Rahabu
Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa.
vipande vipande.
13 pAliisafisha anga kwa pumzi yake;
kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.
14 qHaya ni mambo madogo tu katika matendo yake;
tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu!
Ni nani basi awezaye kuelewa
ngurumo za nguvu zake?”
Copyright information for SwhNEN