Joshua 12
Orodha Ya Wafalme Walioshindwa
1 aHawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:2 bSihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.
Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi. 3 cPia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi ▼
▼Yaani Bahari ya Galilaya.
hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi ▼▼Yaani Bahari Mfu.
), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga. 4 fNayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.
5 gNaye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.
6 hMose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.
7 iHawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:
8 ▼
wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.
24 ▼In order to format the table contained in this verse correctly, it has been necessary to move the content of some adjacent verses into it.
,
knchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):9 lmfalme wa Yeriko | mmoja |
mfalme wa Ai (karibu na Betheli) | mmoja |
10 mmfalme wa Yerusalemu | mmoja |
mfalme wa Hebroni | mmoja |
11 nmfalme wa Yarmuthi | mmoja |
mfalme wa Lakishi | mmoja |
12 omfalme wa Egloni | mmoja |
mfalme wa Gezeri | mmoja |
13mfalme wa Debiri | mmoja |
mfalme wa Gederi | mmoja |
14 pmfalme wa Horma | mmoja |
mfalme wa Aradi | mmoja |
15 qmfalme wa Libna | mmoja |
mfalme wa Adulamu | mmoja |
16 rmfalme wa Makeda | mmoja |
mfalme wa Betheli | mmoja |
17 smfalme wa Tapua | mmoja |
mfalme wa Heferi | mmoja |
18 tmfalme wa Afeki | mmoja |
mfalme wa Lasharoni | mmoja |
19 umfalme wa Madoni | mmoja |
mfalme wa Hazori | mmoja |
20 vmfalme wa Shimron-Meroni | mmoja |
mfalme wa Akishafu | mmoja |
21 wmfalme wa Taanaki | mmoja |
mfalme wa Megido | mmoja |
22 xmfalme wa Kedeshi | mmoja |
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli | mmoja |
23 ymfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori) ▼ ▼Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori. | mmoja |
mfalme wa Goimu katika Gilgali | mmoja |
24 aamfalme wa Tirsa | mmoja |
Copyright information for
SwhNEN