Luke 22:54-71
Petro Amkana Yesu
(Mathayo 26:57-75; Marko 14:53-72; Yohana 18:12-27)
54 aKisha wakamkamata Yesu, wakamchukua, wakaenda naye mpaka nyumbani kwa kuhani mkuu. Lakini Petro akafuata kwa mbali. 55 bWalipokwisha kuwasha moto katikati ya ua na kuketi pamoja, Petro naye akaketi pamoja nao. 56Mtumishi mmoja wa kike akamwona kwa mwanga wa moto akiwa ameketi pale. Akamtazama sana, akasema, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja na Yesu!”57Lakini Petro akakana, akasema, “Ewe mwanamke, hata simjui!”
58 cBaadaye kidogo, mtu mwingine alimwona Petro akasema, “Wewe pia ni mmoja wao!” Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sio mmoja wao!”
59 dBaada ya muda wa kama saa moja hivi, mtu mwingine akazidi kusisitiza, “Kwa hakika huyu mtu naye alikuwa pamoja na Yesu, kwa maana yeye pia ni Mgalilaya.”
60Petro akajibu, “Wewe mtu, mimi sijui unalosema!” Wakati huo huo, akiwa bado anazungumza, jogoo akawika. 61 eNaye Bwana akageuka, akamtazama Petro. Ndipo Petro akakumbuka lile neno ambalo Bwana alimwambia: “Kabla jogoo hajawika leo, utanikana mara tatu.” 62Naye akaenda nje, akalia kwa majonzi.
Walinzi Wamdhihaki Yesu Na Kumpiga
(Mathayo 26:67-68; Marko 14:65)
63 f gWatu waliokuwa wanamlinda Yesu wakaanza kumdhihaki na kumpiga. 64Wakamfunga kitambaa machoni na kumuuliza, “Tabiri! Tuambie ni nani aliyekupiga?” 65 hWakaendelea kumtukana kwa matusi mengi.Yesu Apelekwa Mbele Ya Baraza
(Mathayo 26:59-66; Marko 14:55-64; Yohana 18:28-38)
66 iKulipopambazuka, baraza la wazee wa watu, ▼▼Baraza la wazee hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo Baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu.
yaani viongozi wa makuhani na walimu wa sheria, wakakutana pamoja, naye Yesu akaletwa mbele yao. 67 kWakamwambia, “Kama wewe ndiye Kristo, ▼▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
tuambie.”Yesu akawajibu, “Hata nikiwaambia hamtaamini. 68 mNami nikiwauliza swali, hamtanijibu. 69 nLakini kuanzia sasa, Mwana wa Adamu ataketi mkono wa kuume wa Mungu Mwenye Nguvu.”
70 oWote wakauliza, “Wewe basi ndiwe Mwana wa Mungu?”
Yeye akawajibu, “Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye.”
71 pKisha wakasema, “Tuna haja gani tena ya ushahidi zaidi? Tumesikia wenyewe kutoka kinywani mwake.”
Copyright information for
SwhNEN