Mark 7:20-23
20Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 21 aKwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, 22 btamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. 23Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”
Copyright information for
SwhNEN