Matthew 13:31-32
Mfano Wa Mbegu Ya Haradali
(Marko 4:30-32; Luka 13:18-19)
31 aAkawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa Mbinguni ni kama punje ya haradali, ambayo mtu aliichukua, akaipanda shambani mwake. 32 bIngawa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua ni mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, nao huwa mti mkubwa, hadi ndege wa angani wanakuja na kutengeneza viota katika matawi yake.”
Copyright information for
SwhNEN