Matthew 22:37-40
37 aYesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 bNayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40 cAmri hizi mbili ndizo msingi wa Sheria na Manabii.”
Copyright information for
SwhNEN