Numbers 7
Sadaka Wakati Wa Kuweka Wakfu Maskani Ya Bwana
1 aMose alipomaliza kuisimamisha Maskani, aliitia mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuiweka wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote. 2 bNdipo viongozi wa Israeli, wale wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka. 3 cWalizileta kama matoleo yao mbele za Bwana: magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa, pamoja na maksai kumi na wawili; yaani maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi, na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya Maskani.4 Bwana akamwambia Mose, 5“Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Kukutania. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.”
6Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi. 7 dAliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao, 8 ena pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni. 9 fLakini Mose hakuwapa Wakohathi chochote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, vile walikuwa wanawajibika.
10 gWakati madhabahu yalitiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu. 11 hKwa maana Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.”
12 iYule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda.
13 jSadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, ▼
▼Shekeli 130 za fedha ni sawa na kilo 1.5.
na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, ▼▼Shekeli 70 za fedha ni sawa gramu 800.
vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 14 msinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, ▼▼Shekeli 10 za dhahabu ni sawa na gramu 110.
likiwa limejazwa uvumba; 15 ofahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 16 pmbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 17 q
,
rmaksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu. 18 sSiku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake.
19Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 20sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 21 tfahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 22mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 23 umaksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari.
24 vSiku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zabuloni, alileta sadaka yake.
25 wSadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 26sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 27fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 28mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 29maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.
30 xSiku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni, alileta sadaka yake.
31Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 32sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 33fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 34mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 35maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri.
36 ySiku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake.
37Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 38sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 39 zfahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 40mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 41maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai.
42 aaSiku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, alileta sadaka yake.
43 abSadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 44sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 45 acfahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 46mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 47maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli.
48 adSiku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu, alileta sadaka yake.
49Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 50 aesinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 51 affahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 52mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 53maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi.
54 agSiku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake.
55Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 56 ahsinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 57 aifahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 58mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 59maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.
60 ajSiku ya tisa Abidani mwana wa Gideoni, kiongozi wa watu wa Benyamini, alileta sadaka yake.
61Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 62 aksinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 63 alfahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 64mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 65 ammaksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gideoni.
66 anSiku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, kiongozi wa watu wa Dani, alileta sadaka yake.
67 aoSadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 68 apsinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 69fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 70mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 71maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.
72 aqSiku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa watu wa Asheri, alileta sadaka yake.
73Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 74sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 75fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 76mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 77maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.
78 arSiku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa watu wa Naftali, alileta sadaka yake.
79 asSadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 80sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba; 81fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa; 82mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 83maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Ahira mwana wa Enani.
84 atHizi ndizo zilikuwa sadaka za viongozi wa Israeli madhabahu yalipowekwa wakfu, wakati yalitiwa mafuta: sahani kumi na mbili za fedha, bakuli kumi na mbili za fedha za kunyunyizia, na masinia kumi na mawili ya dhahabu. 85Kila sahani ya fedha ilikuwa na uzito wa shekeli 130, na kila bakuli la fedha la kunyunyizia lilikuwa na uzito wa shekeli sabini. Masinia yote kumi na mawili yalikuwa na uzito wa shekeli 2,400 ▼
▼Shekeli 2,400 za fedha ni sawa na kilo 28.
kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. 86 avSahani kumi na mbili za dhahabu zilizojazwa uvumba zilikuwa na uzito wa shekeli kumi kila moja, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Kwa jumla, sahani za dhahabu zilikuwa na uzito wa shekeli 120. ▼▼Shekeli 120 za dhahabu ni sawa na kilo 1.4.
87Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo dume kumi na wawili na wana-kondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Mbuzi waume kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi. 88 axJumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo dume sitini, mbuzi dume wa mwaka mmoja sitini na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja sitini. Hizi ndizo zilikuwa sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kutiwa mafuta. 89 ay azMose alipoingia kwenye Hema la Kukutania kuzungumza na Bwana, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya Sanduku la Ushuhuda. Mose akazungumza naye.
Copyright information for
SwhNEN