Proverbs 13
Mema Ya Muda Mfupi Na Yale Ya Kudumu
1 aMwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye,bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.
2 bKutoka tunda la midomo yake mtu hufurahia mambo mema,
bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri.
3 cYeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake,
bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia.
4 dMvivu hutamani sana na hapati kitu,
bali nafsi ya mwenye bidii
hutoshelezwa kikamilifu.
5 eMwenye haki huchukia uongo,
bali waovu huleta aibu na fedheha.
6 fHaki humlinda mtu mwadilifu,
bali uovu humwangusha mwenye dhambi.
7 gMtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote;
mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.
8 hUtajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake,
bali mtu maskini hasikii kitisho.
9 iNuru ya mwenye haki hungʼaa sana,
bali taa ya mwovu itazimwa.
10 jKiburi huzalisha magomvi tu,
bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.
11 kFedha isiyo ya halali hupungua,
bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka.
12 lKilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua,
bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima.
13 mYeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi,
bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo.
14 nMafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima,
ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
15Ufahamu mzuri hupata upendeleo,
bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu.
16 oKila mwenye busara hutenda kwa maarifa,
bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake.
17 pMjumbe mwovu huanguka kwenye taabu,
bali mjumbe mwaminifu huleta uponyaji.
18 qYeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu,
bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa.
19 rTarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi,
bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya.
20 sYeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima,
bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara.
21 tBalaa humwandama mtenda dhambi,
bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki.
22 uMtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi,
bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa
kwa ajili ya wenye haki.
23 vShamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi,
bali dhuluma hukifutilia mbali.
24 wYeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe,
bali yeye ampendaye
huwa mwangalifu kumwadibisha.
25 xMwenye haki hula mpaka akaridhisha moyo wake,
bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa.
Copyright information for
SwhNEN