Proverbs 20
1 aMvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi;yeyote apotoshwaye navyo hana hekima.
2 bGhadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba;
yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake.
3 cNi kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi,
bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.
4 dMvivu halimi kwa majira;
kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama
lakini hapati chochote.
5 eMakusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina,
lakini mtu mwenye ufahamu huyachota.
6 fWatu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma,
bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?
7 gMtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,
wamebarikiwa watoto wake baada yake.
8 hWakati mfalme aketipo katika kiti chake cha enzi kuhukumu,
hupepeta ubaya wote kwa macho yake.
9 iNi nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi;
mimi ni safi na sina dhambi?”
10 jMawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti,
Bwana huchukia vyote viwili.
11 kHata mtoto hujulikana kwa matendo yake,
kama tabia yake ni safi na adili.
12 lMasikio yasikiayo na macho yaonayo,
Bwana ndiye alivifanya vyote viwili.
13 mUsiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini,
uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.
14“Haifai, haifai!” asema mnunuzi,
kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.
15 nDhahabu kunayo, na marijani kwa wingi,
lakini midomo inenayo maarifa
ni kito cha thamani kilicho adimu.
16 oChukua vazi la yule awekaye dhamana
kwa ajili ya mgeni;
lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo
kwa ajili ya mwanamke mpotovu.
17Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu,
bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe.
18 pFanya mipango kwa kutafuta mashauri,
ukipigana vita, tafuta maelekezo.
19 qManeno ya kusengenya husababisha kutokuaminika,
kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi.
20 rIkiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake,
taa yake itazimwa katika giza nene.
21 sUrithi upatikanao haraka mwanzoni,
hautabarikiwa mwishoni.
22 tUsiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!”
Mngojee Bwana, naye atakuokoa.
23 u Bwana anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu,
nazo mizani zisizo halali hazimpendezi.
24 vHatua za mtu huongozwa na Bwana.
Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe?
25 wNi mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka
na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.
26 xMfalme mwenye hekima hupepeta waovu,
hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.
27 yTaa ya Bwana huchunguza roho ya mwanadamu,
huchunguza utu wake wa ndani.
28 zUpendo na uaminifu humweka mfalme salama,
kwa njia ya upendo, kiti chake cha enzi huwa salama.
29 aaUtukufu wa vijana ni nguvu zao,
mvi ni fahari ya uzee.
30 abMapigo na majeraha huusafisha ubaya,
nayo michapo hutakasa utu wa ndani.
Copyright information for
SwhNEN