‏ Proverbs 31:19-24

19Huweka mikono yake kwenye pia,
navyo vidole vyake hushikilia kijiti chenye uzi.
20 aHuwanyooshea maskini mikono yake
na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.
21 bTheluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake,
kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.
22Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake,
yeye huvaa kitani safi na urujuani.
23 cMume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji,
aketipo miongoni mwa wazee wa nchi.
24Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza,
naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.
Copyright information for SwhNEN