Psalms 1

KITABU CHA KWANZA

(Zaburi 1–41)

Furaha Ya Kweli

1 aHeri mtu yule ambaye
haendi katika shauri la watu waovu,
wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,
au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
2 bBali huifurahia sheria ya Bwana,
naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.
3 cMtu huyo ni kama mti uliopandwa
kando ya vijito vya maji,
ambao huzaa matunda kwa majira yake
na majani yake hayanyauki.
Lolote afanyalo hufanikiwa.

Huzuni Ya Waovu

4 dSivyo walivyo waovu!
Wao ni kama makapi
yapeperushwayo na upepo.
5 eKwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,
wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.

6Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki,
bali njia ya waovu itaangamia.
Copyright information for SwhNEN