Psalms 109

Lalamiko La Mtu Aliyeko Kwenye Shida

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1 aEe Mungu, ambaye ninakusifu,
usiwe kimya,
2 bkwa maana watu waovu na wadanganyifu
wamefungua vinywa vyao dhidi yangu;
wasema dhidi yangu
kwa ndimi za udanganyifu.
3 cWamenizunguka kwa maneno ya chuki,
wananishambulia bila sababu.
4 dWanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki,
lakini mimi ninawaombea.
5 eWananilipiza mabaya kwa mema,
chuki badala ya urafiki wangu.

6 fAgiza mtu mwovu ampinge,
mshtaki
Mshtaki hapa maana yake ni Shetani.
asimame mkono wake wa kuume.
7 hAnapohukumiwa, apatikane na hatia,
nayo maombi yake yamhukumu.
8 iSiku zake za kuishi na ziwe chache,
nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine.
9 jWatoto wake na waachwe yatima,
mke wake na awe mjane.
10 kWatoto wake na watangetange wakiomba,
na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao.
11 lMtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo,
matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni.
12 mAsiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema
wala wa kuwahurumia yatima wake.
13 nUzao wake na ukatiliwe mbali,
majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho.
14 oMaovu ya baba zake na yakumbukwe
mbele za Bwana,
dhambi ya mama yake
isifutwe kamwe.
15 pDhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana,
ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani.

16 qKwa maana kamwe hakuweza kutenda wema,
bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,
aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo.
17 rAlipenda kulaani,
nayo laana ikampata;
hakupenda kubariki,
kwa hiyo baraka na ikae mbali naye.
18 sAlivaa kulaani kama vazi lake,
nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji,
kwenye mifupa yake kama mafuta.
19 tNa iwe kama joho alilozungushiwa,
kama mshipi aliofungiwa daima.
20 uHaya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu,
kwa wale wanaoninenea mabaya.

21 vLakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi,
unitendee wema kwa ajili ya jina lako,
uniokoe kwa wema wa pendo lako.
22Maana mimi ni maskini na mhitaji,
moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
23 wNinafifia kama kivuli cha jioni,
nimerushwa-rushwa kama nzige.
24 xMagoti yangu yamelegea kwa kufunga,
mwili wangu umedhoofika na kukonda.
25 yNimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu,
wanionapo, hutikisa vichwa vyao.

26 zEe Bwana, Mungu wangu nisaidie,
niokoe sawasawa na upendo wako.
27 aaWatu na wafahamu kuwa ni mkono wako,
kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili.
28 abWanaweza kulaani, lakini wewe utabariki,
watakaposhambulia wataaibishwa,
lakini mtumishi wako atashangilia.
29 acWashtaki wangu watavikwa fedheha,
na kufunikwa na aibu kama joho.

30 adKwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana,
katika umati mkubwa nitamsifu.
31 aeKwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji,
kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu.
Copyright information for SwhNEN