Psalms 115:4-8
4 aLakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5 bZina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
6zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
zina pua, lakini haziwezi kunusa;
7zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,
zina miguu, lakini haziwezi kutembea;
wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
8 cWale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
Copyright information for
SwhNEN