Psalms 143
Maombi Ya Kuokolewa Dhidi Ya Adui
Zaburi ya Daudi.
1 aEe Bwana, sikia sala yangu,sikiliza kilio changu unihurumie;
katika uaminifu na haki yako
njoo unisaidie.
2 bUsimhukumu mtumishi wako,
kwa kuwa hakuna mtu anayeishi aliye mwenye haki mbele zako.
3 cAdui hunifuatilia,
hunipondaponda chini;
hunifanya niishi gizani
kama wale waliokufa zamani.
4 dKwa hiyo roho yangu inazimia ndani yangu,
moyo wangu ndani yangu unakata tamaa.
5 eNakumbuka siku za zamani;
natafakari juu ya kazi zako zote,
naangalia juu ya kazi
ambazo mikono yako imezifanya.
6 fNanyoosha mikono yangu kwako,
nafsi yangu inakuonea kiu kama ardhi kame.
7 gEe Bwana, unijibu haraka,
roho yangu inazimia.
Usinifiche uso wako,
ama sivyo nitafanana na wale washukao shimoni.
8 hAsubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma,
kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako.
Nionyeshe njia nitakayoiendea,
kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu.
9 iEe Bwana, uniokoe na adui zangu,
kwa kuwa nimejificha kwako.
10 jNifundishe kufanya mapenzi yako,
kwa maana wewe ndiwe Mungu wangu,
Roho wako mwema na aniongoze
katika nchi tambarare.
11 kEe Bwana, kwa ajili ya jina lako, hifadhi maisha yangu,
kwa haki yako nitoe katika taabu.
12 lKwa upendo wako usiokoma,
nyamazisha adui zangu;
waangamize watesi wangu wote,
kwa kuwa mimi ni mtumishi wako.
Copyright information for
SwhNEN