Psalms 147:15-18
15 aHutuma amri yake duniani,
neno lake hukimbia kasi.
16 bAnatandaza theluji kama sufu
na kutawanya umande kama majivu.
17 cHuvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe.
Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake?
18 dHutuma neno lake na kuviyeyusha,
huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka.
Copyright information for
SwhNEN